Swenani wrote:masukuma wrote:but Obama's inauguration was quite something!! as waswahili would say it. Halaiki ya watu; Umati wa watu;, Hadhara kuu ya watu; Sisisi ya watu; Sufufu ya watu! Wengi waliompigia Kura Trump hawawezi panda ndege kuenda jimbo lingine ilikushuhudia uzinduzi wa uraisi wa Trump. Usisahau D.C. ndio jimbo ambalo chama cha Democrats kiko na ushawishi mkuu ukilinganishwa na majimbo mengine.
Hicho/hiyo kiswahli jameni...kwa kweli umetekenywa na nyege za uswahilini kaka braza
kaka, usistajabu kinywa wazi. Ukistaajabu vya Musa utaona vya Firauni! nimehariri aya na kurekebisha!! sasa ya soma hivi!!
Quote:but Obama's inauguration was quite something!! as waswahili would say it. Halaiki ya watu; Umati wa watu; Hadhara kuu ya watu; Sisisi ya watu; Sufufu ya watu! Wengi waliompigia Kura Trump hawawezi kuabiri ndege kuenda jimbo lingine ilikushuhudia uzinduzi wa uraisi wa Trump. Nauli ni ghali mno kwa watu hawa. Usisahau D.C. ndio jimbo ambalo chama cha Democrats kiko na ushawishi mkuu ukilinganishwa na majimbo mengine.
ukweli ni kwamba - wapiga kura wengi wa Trump ni wale kwa kimombo twawaita "deplorables". wengine hawana kazi wala bazi! Wengi wao walitimuliwa kazini wakati viwanda vilihamishwa. jambo la kushangaza na ambalo kwangu ni kejeli kuu kwenye mambo haya tunayo shuhudia ni kuwa - baraza la mawaziri la Trump ni la mabwenyenye! Trump mwenyewe ni bwenyenye! wahenga walinena wakisema "kiatu usicho kivaa hujui kinabana wapi"! sielewi vile hawa mabwenyenye wata elewa matatizo ya wale "deplorables". Trump mwenyewe ni mjeuri!! hasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini - yeye aamini ya kuwa yeye ni mwerevu mno. je? atawezaje kutibu uchungu ambao haujui?
All Mushrooms are edible! Some Mushroom are only edible ONCE!