Don't shoot the messenger.
In summary this Tanzanian author makes some points:
- Supporting foreign leagues benefits European economies at the expense of our local economies
- Supporting foreign leagues puts yet more money into the coffers of European teams thus increasing the gap between European football and African football
- Supporting foreign league amounts to a continuation of colonial rule by the Europeans
- It is the reason many of Africa’s former players are flat broke mitaani while their Euro counterpart retire to their beach front homes
- Supporting foreign leagues is the reason local teams find it impossible to find sponsorship. All the sponsors flock to be associated with European football
- Local newspapers give more space to European leagues
- Locals wear jerseys of the European teams thus putting yet more money into the coffers of European teams
- Africans now want to be known as Wazungu weusi
Quote:
Ni wikiendi moja tukiwa katiba banda la kutazama Soka mtaani kwangu. Naposema kutazama mpira namaanisha huu wa Ulaya uliozoeleka hadi vijijini kuliko mpira wetu wa Kiafrika, au Butua Butua kama waanvyoita.
Timu moja inapata goli na wananchi 'washabiki' wake wanaruka kwa furaha huku wenzao waliofungwa wakinywea kwa huzuni.
Mjadala juu ya mchezo ule unaendelea mtaani, watu wanataniana na kushiriki pamoja furaha ya timu 'yao' kushinda.
Mpira ndio umekuwa ulevi wa kisasa, watu wengi hutazama Soka. Zamani kidogo hali ilikuwa tofauti, watu wachache tu, tena wanaume, waliokuwa wakipoteza muda wao maridhawa kupigizana kelele kuhusu Soka. Sasa hivi hali ni tofauti, wanawake na vijana wadogo kiumri wamekuwa wadau wakubwa wa Soka la kwenye televisheni.
Kupanuka kwa teknolojia ya habari na kukua kwa makampuni yanayoonesha ligi za Ulaya
kama DSTv kumefanya hali iwe kama ilivyo.
Mpira ni mchezo maarufu duniani kote na unavutia kutazama, Brazil, ambako kunaaminika homa ya Soka iko juu wana neno Joga Bonito ambalo tafsiri yake ni 'mchezo unaovutia' kumaanisha umaridadi wa mchezo huu.
Takwimu ambazo si rasmi zinaonesha kuwa umakini katika Soka la nyumbani unapungua, au tuseme idadi ya watu ambao humakinikia Soka la ulaya inaongezeka kila kukicha. Hali hii iko Tanzania na nchi zingine za Kiafrika.
Athari hii haipo Afrika au katika Soka pekee, bali pia kwa nchi za Amerika Kusini na Karibea ambako wao ni washabiki wakubwa wa Ligi ya Baseball ya Marekani (Major League Baseball)
Jambo hili lina manufaa makubwa sana kwa uchumi wa timu na nchi husika ambao wana ligi yao. Upande wa pili ni maumivu na kuendelea kukandamizwa kiuchumi.
Athari ya moja kwa moja kiuchumi ni pale ambapo washabiki wanaponunua jezi na wakati mwingine kulipia uanachama wa timu za Ulaya. Kwa maneno rahisi ni kuwa wanatoa pesa nchini na kupeleka Ulaya, jambo ambalo si zuri kiuchumi.
Athari nyingine kubwa ni pale ambako tunawachangia fedha kupitia haki za matangazo. Mchakato wa haki za matangazo si mgeni sana machoni kwa Watanzania kwani mwanzo mwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara tulishuhudia kitu cha aina hii baina ya Azam Media na timu za Ligi Kuu.
Timu huwa zinalipwa na kampuni za matangazo ya televisheni, kisha wao hupata faida kwa kuwauzia watazamaji matangazo hayo. Hapa Afrika kampuni ya DSTv ndio huonesha ligi nyingi za Ulaya, na huuza huduma zake kwa bei ya juu sana (pengine kuliko kampuni yoyote hapa nchini).
Kwa nchi ambako watu wake wanaishi chini ya dola moja kuendelea kuchangia uchumi mkubwa wa vilabu vya Ulaya inasikitisha, ingawa ukweli huu hausemwi siku zote. Ni muendelezo wa ukoloni mamboleo kwani Waafrika wanatawaliwa na Soka na michezo mingine.
Watu wengi huwalaumu wachezaji wa zamani ambao hali zao za kiuchumi zimeyumba. Washabiki hao hao ndio wanaona afadhali kuchangia tiumu ya Ulaya kuliko kwenda uwanjani na kuchangia timu za ndani.
Katika hali ambapo mechi za Ulaya zinaoneshwa na kushabikiwa nchini mwetu, washabiki wa Soka hutakiwa kuchagua kati ya mechi za nyumbani au za kigeni.
Kuna kipindi ratiba ya Ligi Kuu Uganda ilikuwa inapangwa ili kukwepa kugongana na ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza. Hapa nchini si jambo geni kuona watu wakiingia na redio viwanjani ili kupata matokeo ya mechi za Ulaya na kinyume chake.
Katika hali ya kuelekea mapinduzi ya michezo, hatuwezi kufanikiwa kama watu wataendelea kuwa washabiki wa michezo ya Ulaya. Timu zinahitaji washabiki ili ziendelee kudumu na zipate udhamini kutoka kwa makampuni. Simba na Yanga zilipata udhamini mnono kutoka TBL sio tu kwa kuwa wana kiwango kikubwa, lakini pia kwa kuwa wana idadi kubwa ya mashabiki ambao ndipo ,soko la bidhaa lilipo.
Vyombo vya habari na wachambuzi wa michezo nao wamefuata mkumbo huu. Magazeti mengi yamejaa habari za michezo za nje kuliko ya ndani na wachambuzi hutumia misuli mingi kuelezea na kufafanua yanayohusu timu za Ulaya.
Hali hii imepelekea hata washabiki nao kutojali sana kama tunadidimia. Wapo watu ambao huumia zaidi timu zao za Ulaya zinapofungwa kuliko inapofungwa timu yetu ya Taifa.
Mauzo ya jezi pia yamehamia kwa timu za Ulaya, na sio za nyumbani. Bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni kuzigandamiza timu zetu wenyewe ambazo mafanikio yazo ni heshima kwetu.
Ushabiki wa Kizungu ukizidi sana ndipo madhara ya waziwazi huonekana. Nchini Kenya kwa mfano, mechi kati ya Gor Mahia na Leopards iliyochezwa Mei mwaka jana ilihudhuriwa na washabiki 7000 tu katika uwanja wa Kasarani ambao una uwezo wa kuingiza watu 60'000.
Katika ligi yetu hapa Tanzania mahudhurio sio mabaya sana kwani hata mechi ambazo hazihusishi timu kongwe za Simba na Yanga inaweza kujaza uwanja (mfano Azam vs Mbeya City, Chamazi)
ulimbukeni wa michezo ya Ulaya unaenda mbali kiasi cha watu kujinyonga kisa timu ya Ulaya (Kenya) na tukio la shabiki mmoja wa Nigeria kugonga wenzake na gari baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Michezo ni utambulisho wa utamaduni, na inaonekana kuwa Waafrika wameamua kutambulika kama 'wazungu weusi'. Ndio, ni rahisi kusikia mtu akijitambulisha kuwa yeye ni shabiki damu wa Barcelona na tumu 'yake' ikifungwa hana raha.
Wenzetu kwa kufahamu madhaifu yetu wanazidi kutukoleza kwa kujifanya wanatujali. Mara kadhaa tumeona ziara za makombe ya Ligi za Ulaya yakifanya ziara Afrika. Ziara hizi hazifanywi kwa mapenzi yao kwetu bali mahitaji ya kibiashara na kuzidi kututeka akili.
Masikini mtu kwao, naamini ipo siku weusi wenzangu watatambua nafasi yao katika kuoko michezo na kuamua kurudi nyumbani.