SHERIA NA MASHARTI.
ZIFUATAZO NI ADHABU ZITOLEWAZO KWA UVUNJAJI WA SHERIA ZA CHAMA CHA
WANYWAJI POMBE na Bw. MUTHUTHO:
1. Kosa la kumtoroka mlevi mwenzako kwenye bar - Jela miezi tisa.
2. Kuacha kunywa pombe na fedha unazo - Kifungo cha maisha.
3. Kuvunja chupa ya beer - Jela miaka miwili.
4. Kumkaribisha mume au mke wa rafiki yako bila idhini yake - Viboko ishirini vya makalio na kufungiwa kunywa nusu siku.
5. Kumchukulia dhamana mtu asiyepiga mma(pombe) - Adhabu yake ni kufukuzwa/kutolewa chamani.
6. Kumwibia pombe mlevi mwenzako ni kosa kubwa - Jela mwaka mmoja.
7. Kukataa kunywa wakati umekaribishwa - Jela miaka mitano.
8. Kukwepa ulevi wa aina yoyote - adhabu ni Kunyang'anywa mume au mke, kama huna basi utaozwa mume au mke kwa nguvu.
9. Kupita Bar au Grocery na kujifanya huoni hilo ni kosa kubwa linalostahili faini ya kuwanunulia wanywaji wote waliokuwa kwenye
Grocery au Bar kila mtu kinywaji anachokunywa na kukaa ukiwaangalia mpaka wamalize.
10. Kumcheka mnywaji mwenzako akiwa amelewa ni kosa la jinai, unachotakiwa kufanya ni kumpongeza kwa kazi nzito aliyoifanya. Adhabu yake ni - Kutolewa kwenye Bar kwa muda wa dakika moja.
Life is like playing a violin solo in public and learning the instrument as one goes on.